• HABARI MPYA

  Saturday, June 29, 2019

  BAFANA BAFANA YAFUFUA MATUMAINI YA KUSONGA MBELE AFCON

  BAO pekee la nyota wa Amiens SC ya Ufaransa, Bongani Zungu dakika ya 68 lilitosha kuipa Afrika Kusini ushindi wa 1-0 dhidi ya Namibia katika mchezo wa Kundi Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Uwanja wa Al Salam mjini Cairo.
  Kwa ushindi huo, Bafana Bafana inajipatia pointi tatu za kwanza baada ya kufungwa 1-0 Ivory Coast  kwenye mchezo wa kwanza kuelekea mchezo wake wa mwisho dhidi ya Morocco keshokutwa.
  Morocco sasa ndiyo inaongoza kundi D baada ya jana kuifunga Ivory Coast 1-0, bao pekee la nyota wa Leganes ya Hispania, Youssef En-Nesyri dakika ya 23 Uwanja wa Al Salam mjini Cairo, hivyo kufikisha pointi sita, wakati Namibia ambayo haina pointi inashika mkia.   Bongani Zungu amefufua matumaini ya Bafana Bafana kwenda hatua ya 16 Bora

  Mchezo mwingine wa jana ulikuwa wa Kundi E uliomalizika kwa sare ya 1-1 Uwanja wa New Suez, Mali wakitangulkia kwa bao la Diadie Samassekou dakika ya 60 kabla ya Wahbi Khazri kuisawazishia Tunisia dakika ya 70.
  Mali sasa inaongoza Kundi E kwa pointi zake nne, ikifuatiwa na Tunisia pointi mbili, Angola pointi moja na Mauritania ambayo haina pointi hata moja inashika mkia.
  Michuano hiyo inaendelea kwa mechi nyingine tatu ikiwemo ya Kundi E kati ya Mauritania na Angola kuanzia Saa 11:30 jioni ikifuatiwa ne mechi za Kundi F kati ya Cameroon na Ghana Saa 2:00 usiku na Benin na Guinea-Bissau Saa 5:00 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BAFANA BAFANA YAFUFUA MATUMAINI YA KUSONGA MBELE AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top