• HABARI MPYA

  Thursday, June 20, 2019

  AMBOKILE WA MBEYA CITY ATUA TP MAZEMBE KUCHUKUA NAFASI YA IBRAHIM AJIBU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI chipukizi wa Tanzania, Eliud Ambokile yuko mbioni kujiunga na klabu ya Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). 
  Klabu yake, Mbeya City leo imethibitisha kuwa kwenye mazungumzo na TP Mazembe kuhusu nyota huyo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
  “Tunathibitisha kuwepo kwa mazungumzo kati yetu na klabu ya TP. Mazembe kuhusu nyota wetu Eliud Ambokile. Taarifa zaidi kuhusu makubaliano husika na kandarasi ya Eliud Ambokile itatolewa hivi karibuni. -Ofisi ya Habari,”imesema taarifa ya Mbeya City.

  Eliud Ambokile anakwenda TP Mazembe baada ya mipango ya kuchezea Black Leopards FC ya Afrika Kusini kukwama 

  Januari mwaka huu Ambokile alijiunga na klabu ya Black Leopards FC ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini kwa mkopo wa miezi mitatu, baada ya mpango wa awali wa kujiunga na El Gounah ya Misiri kushindikana.
  Hata hivyo, mambo hayakumuendea vizuri Black Leopards Ambokile akaamua kurejea Mbeya na sasa anapata nafasi nyingine kwenda nje kujaribu tena bahati yake.
  Ikiumbukwe, Mazembe awali ilikuwa inataka kumsajili mchezaji mwingine Mtanzania, Ibrahim Ajibu ambaye misimu miwili iliyopita alikuwa Yanga SC, lakini akagoma na habari zinasema amerejea klabu yake ya zamani, Simba SC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AMBOKILE WA MBEYA CITY ATUA TP MAZEMBE KUCHUKUA NAFASI YA IBRAHIM AJIBU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top