• HABARI MPYA

  Monday, June 17, 2019

  NI YANGA NA AZAM FC NA SIMBA SC NA MTIBWA SUGAR NUSU FAINALI LIGI KUU YA VIJANA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC itakutana na Azam FC katika Nusu Fainali ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, wakati mahasimu wao jadi, Simba SC watakutana na Mtibwa Sugar.
  Hiyo ni baada ya mechi za mwisho za Kundi B leo,  Mtibwa Sugar na Azam FC zikigawana pointi kwa sare ya 1-1 na Tanzania Prisons ikiichapa 2-1 Biashara United.
  Kwa matoko hayo, Mtibwa Sugar wanamaliaza kileleni mwa kundi hilo ikiwa na pointi saba sawa na Azam FC , lakini timu ya Manungu inakuwa juu kwa wastani wake mzuri wa mabao.

  Tanzania Prisons wamemaliza nafasi ya tatu kwa pointi zao tatu na Biashara United wameburuza mkia wakiwa hawajaambulia pointi yoyote.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI YANGA NA AZAM FC NA SIMBA SC NA MTIBWA SUGAR NUSU FAINALI LIGI KUU YA VIJANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top