• HABARI MPYA

  Sunday, June 23, 2019

  RAIS DK. MAGUFULI AKUTANA NA MDHAMINI WA KLABU YA SIMBA, MZEE HAMISI KILOMONI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli leo amepata fursa ya kukutana na kuzungumza kwa uchache na Mdhamini wa klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam, Mzee Hamisi Kilomoni.
  Rais Magufuli, kipenzi cha Watanzania alikutana na Mzee Kilomoni leo nyumbani kwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Abdallah Sadalla ‘Mabodi’ mjini Dar es Salaam.
  Rais Magufuli alikuwa amekwenda kumpa pole Dk. Abdallah Sadalla ‘Mabodi’ ambaye amefiwa na mkewe, Dk. Badria Abubaker Gunar aliyefariki dunia jana mjini Dar es salaam.

  Rais Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na Mdhamini wa klabu ya Simba SC, Mzee Hamisi Kilomoni leo mjini Dar es Salaam

  Na Rais Magufuli alimfuata Mzee Kilomoni alipokuwa ameketi na kumpa mkono kumsabahi kabla ya kuzungumza naye mawili matatu na kuagana. 
  Rais Magufuli pia leo alikwenda kumpa pole, Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga, Tarimba Abbas ambaye amefiwa na wanawe wawili wa kiume mfululizo hivi karibuni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS DK. MAGUFULI AKUTANA NA MDHAMINI WA KLABU YA SIMBA, MZEE HAMISI KILOMONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top