• HABARI MPYA

  Monday, June 17, 2019

  MAKONDA AAHIDI KUWAKABIDHI YANGA SC ENEO LA KUJENGA UWANJA IJUMAA KIGAMBONI

  Na Asha Said, DAR ES SALAAM
  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameahidi kuikabidhi klabu ya Yanga eneo la kujenga Uwanja Ijumaa wiki hii.
  Makonda ameyasema hayo leo hoteli  ya Serena mjini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa Habari, kufuatia kukutanana viongozi wa Yanga chini ya Mwenyekiti Dk. Mshindo Msolla.
  Makonda ametimiza ahadi yake ya Jumamosi kwenye tamasha la kuichangia klabu ya Yanga “Kubwa Kuliko” kwa kukutana na viongozi wa klabu hiyo kuzungumzia kuwapa eneo Kigamboni.
  Makonda alisema makabidhiano hayo yatafanyika Ijumaa baada ya kukamilisha usajili wa eneo hilo ambalo ni mchango wake kwa ahadi Jumamosi Diamond Jubilee.Alisema tayari ameshapata nyaraka mbalimbali na sasa anasubiri nakala ya Katiba ya klabu hiyo ili aweze kukamilisha zoezi hilo, kwani anataka Yanga ndio iwe mmiliki wa eneo na si mtu. 
  “Ijumaa nitakabidhi eneo la Yanga. Ninaamini kila kitu kitakuwa kimekamilika, hivyo hakutakuwa na sababu ya kushindwa kuliona eneo hilo," alisema Makonda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAKONDA AAHIDI KUWAKABIDHI YANGA SC ENEO LA KUJENGA UWANJA IJUMAA KIGAMBONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top