• HABARI MPYA

  Saturday, June 22, 2019

  MISRI WAANZA VYEMA AFCON 2019, YAIPIGA ZIMBABWE 1-0 CAIRO

  WENYEJI, Misri wameanza vyema Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Zimbabwe usiku wa Ijumaa Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Mahmoud Ibrahim Hassan maarufu kwa jina la utani, Trezeguet anayechezea klabu ya Kasımpasa ya Uturuki aliyefunga dakika ya 41 akimalizia pasi ya beki wa Al Ahly ya nyumbani, Ayman Ashraf . 
  Matokeo hayo yanamaanisha kikosi cha kocha Mmexico, Javier Aguirre Onaindia kinaanza vyema kuwania taji la nane la AFCON baada ya awali kulibeba katika miaka ya 1957, 1959, 1986, 1998, 2006, 2008 na 2010.
  Trezeguet (wa pili kushoto) akishangilia baada ya kuifungia bao pekee Misri ikiilaza Zimbabwe 1-0

  Mshambuliaji ws Liverpool, Mohamed Salah aliwekewa ulinzi mkali na wachezani wa Zimbabwe kiasi cha kushindwa kufurukuta leo. 
  Kesho kutakuwa na mechi mbili, ya Kundi A Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikimenyana na Uganda kuanzia Saa 11:30 itakayofuatiwa na za Kundi B Nigeria dhidi ya Burundi Saa 2:00 usiku na Guinea na Madagascar Saa 5:00 usiku.
  Taifa Stars itatupa kete yake ya kwanza jumapili kwa kumenyana na Simba wa Teranga kuanzia Saa 2:00 usiku, itakayofuatiwa na mchezo mwingine wa kundi hilo kati ya Algeria na Kenya Saa 5:00 usiku, ambazo zitatanguliwa na mechi ya Kundi D kati ya Morocco na Namibia Saa 11:30 jioni.
  Kikosi cha Misri kilikuwa; Mohamed El Shenawy, Ahmed Hegazi, Ayman Ashraf, Mahmoud Alaa, Ahmed El Mohamady, Abdalla El Said/, Tarek Hamed, Mohamed Elneny, Trezeguet/, Mohamed Salah na Marwan Mohsen.
  Zimbabwe; Edmore Sibanda/Evans, Tendayi Darikwa, Teenage Hadebe, Divine Lunga, Ovidy Karuru, Knowledge Musona/Talent Chawapiwa dk85, Khama Billiat, Alec Mudimu, Marvelous Nakamba, Marshall Munetsi na Nyasha Mushekwi/Evans Rusike dk81.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MISRI WAANZA VYEMA AFCON 2019, YAIPIGA ZIMBABWE 1-0 CAIRO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top