• HABARI MPYA

  Wednesday, June 19, 2019

  SIMBA NA YANGA KUKUTANA TENA LIGI YA VIJANA, AZAM FC NA MTIBWA ZATINGA FAINALI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU za Azam FC na Mtibwa Sugar zitakutana katika fainali ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 Ijumaa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
  Hiyo ni baada ya timu hizo kuwatoa wapinzani wao, Simba na Yanga katika mechi za Nusu Fainali leo hapo hapo Uwanja wa Azam Complex.
  Ilianza Azam FC kuitoa Yanga kwa penalti 3-0 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90, kabla ya Mtibwa Sugar kuichapa Simba SC 3-1.     
  Baada ya kutawala mchezo ndani ya dakika 90 huku wakishindwa kutumia vyema nafasi nzuri walizotengeneza, Yanga walikwenda kukosa penalti zote tatu za mwanzo na kutolewa kiulaini.

  Mtibwa Sugar wao walitoka nyuma baada ya kutanguliwa na bao la Modest Modest aliyeitangulzia SImba SC dakika ya sita na kushinda kwa mabao ya Onesmo Mayaya dakika ya 21 na 84 na Joseph Mkele dakika ya 48.
  Wakati Azam FC itakutana na Mtibwa Sugar katika fainali, Simba na Yanga watakutana katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu mapema Ijumaa Azam Complex.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA NA YANGA KUKUTANA TENA LIGI YA VIJANA, AZAM FC NA MTIBWA ZATINGA FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top