• HABARI MPYA

  Friday, June 28, 2019

  YANGA SC YAVAMIA KAMBI ZA AFCON MISRI NA KUSAJILI KIPA WA KENYA NA BEKI WA TAIFA STARS

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Yanga SC imesajili wachezaji wawili wapya, kipa Mkenya Farouk Shikalo na beki Mtanzania, Ally Mtoni ‘Sonso’ ambao wapo na timu zao za taifa kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2019 zinazoendelea nchini Misri. 
  Picha zimevuja wachezaji hao wawili wakiwa na kiongozi wa Yanga SC wanasaini mikataba leo mjini Cairo siku moja tu baada ya timu zao kukutana katika mchezo wa Kundi C jana.
  Shikalo, kipa wa Bandari ya Mombasa na Sonso beki wa Lipuli FC ya Iringa wote walikuwa benchi kama wachezaji wa akiba timu zao zikimenyana katika mchezo wa Kundi C AFCON 2019, Kenya wakiibuka na ushindi wa 3-2.
  Yanga SC ilivutiwa na Shikalo baada ya kumuona kwenye michuano ya SportPesa Super Cup akiwa na Bandari, wakati Sonso ilikumbana naye katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
  Kipa Mkenya, Farouk Shikalo (kulia) akisaini mkataba wa kujiunga na Yanga SC kwenye kambi ya Harambee Stars mjini Cairo   

  Beki Ally Mtoni ‘Sonso’ akisaini mkataba wa kujiunga na Yanga kwenye kambi ya Taifa Stars mjini Cairo 

  Pamoja na wawili hao, kuna taarifa Yanga SC pia ilikuwa inawania saini ya mchezaji mwingine wa akiba wa Taifa Stars, kipa Metacha Boniface Mnata.   
  Wawili hao wanafanya idadi ya wachezaji wapya waliosajiliwa Yanga hadi sasa kufika 12, kati ya hao wane tu ndiyo wazawa ambao mabeki Sonso, Ally Ally kutoka KMC ya Kinondoni, viungo Abdulaziz Makame kutoka Mafunzo ya Zanzibar na Mapinduzi Balama kutoka Alliance FC ya Mwanza.
  Wengine wote ni wageni ambao ni Sadney Urikhob kutoka Namibia, Lamine Moro kutoka Ghana, Juma Balinya kutoka Uganda, Issa Bigirimana, Patrick Sibomana wote wa Rwanda, Mustapha Seleman kutoka Burundi na Maybin Kalengo kutoka Zambia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAVAMIA KAMBI ZA AFCON MISRI NA KUSAJILI KIPA WA KENYA NA BEKI WA TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top