• HABARI MPYA

  Tuesday, June 25, 2019

  IVORY COAST NA MALI NAZO ZAANZA VYEMA MICHUANO YA AFCON

  BAO pekee la Jonathan Kodjia limeipa mwanzo mzuri Ivory Coast katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2019 baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa Kundi D Jumatatu Uwanja wa Al Salam mjini Cairo, Misri.
  mshambuliaji huyo wa Aston Villa ya England alifunga bao hilo dakika ya 64 akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji wa Toulouse ya Ufaransa, Max-Alain Gradel.
  Ushindi huo unawafanga Tembo wa Ivory Coast waanzie kileleni mwa Kundi D wakilingana kwa pointi na Morocco ambayo jana iliipiga 1-0 Namibia ambayo kama Afrika Kusini wanaeleka kwenye michezo ya pili wakiwa na maumivu ya vipigo vinavyofanana.

  Jonathan Kodjia akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Ivory Coast bao pekee la ushindi 

  Aidha, katika mchezo wa Kundi E, Mali iliibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Mauritania Uwanja wa New Suez.
  Mabao ya Mali yalifungwa na washambuliaji Abdoulay Diaby wa Sporting Lisbon dakika ya 37, Moussa Marega wa FC Porto zote za Ureno kwa penalti dakika ya 45, kiungo Adama Traore II wa Cercle Brugge ya Ubelgiji dakika ya 55 na 73 wakati la vibonde wao lilifungwa na kiungo wa Real Valladolid ya Hispania, Moctar Sidi El Hacen kwa penalti dakika ya 72.
  Nayo Tunisia ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Angola katika mchezo mwingine wa Kundi E, Uwanja wa New Suez . Tunisia walitangulia kwa bao la mshambuliaji wa AS Eupen ya Ubelgiji, Youssef Msakni kwa penalti dakika ya 34, kabla ya mshambuliaji wa Alanyaspor ya Uturuki, Djalma Campos kuisawazishia Angola dakika ya 73.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IVORY COAST NA MALI NAZO ZAANZA VYEMA MICHUANO YA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top