• HABARI MPYA

  Sunday, June 02, 2019

  ANTHONY JOSHUA ACHAKAZWA MAREKANI, APIGWA KWA KO NA RUIZ

  Bondia Muingereza Anthony Joshua akiwa chini baada ya kuangushwa na mpinzani wake, Mmarekani mwenye asili ya Mexico, Andy Ruiz Jr Alfajiri ya leo ukumbi Madison Square Garden mjini New York kwenye pambano la uzito wa juu. Joshua amevuliwa ubingwa wa dunia wa uzito wa juu duniani baada ya kupigwa kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya saba. Ruiz hajawahi kuangushwa kabla, lakini naye leo alikalishwa chini raundi ya tatu, kabla ya kuinuka na kuendelea.
  Joshua mwenye urefu wa futi sita atajaribu kurejesha mataji yake ya IBF, WBA na WBO katika pambano la marudiano Novemba. Hilo ni pambano la kwanza Joshua kupoteza baada ya kushinda mapambano yake yote 22 ya awali, 21 kwa knockout, wakati Ruiz mwenye urefu wa futi nne ameshinda pambalo la 32 na 22 kwa KO, huku akiwa amepoteza pambano moja pia 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ANTHONY JOSHUA ACHAKAZWA MAREKANI, APIGWA KWA KO NA RUIZ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top