• HABARI MPYA

  Saturday, May 19, 2018

  YANGA YA SASA NI ‘KICHWA CHA MWENDAWAZIMU’…LEO IMEPIGWA 1-0 NA MWADUI SHINYANGA

  Na Mwandishi Wetu, SHINYANGA
  YANGA SC leo imekamilisha mechi tisa bila ushindi tangu iachwe na kocha wake, Mzambia George Lwandamina baada ya kufungwa 1-0 na Mwadui FC Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Katika mchezo huo wa jioni, bao pekee la Mwadui FC limefungwa na kiungo chipukizi Awesu Ally dakika ya 19 akitumia makosa ya mabeki wa Yanga.
  Yanga ilishinda mara ya mwisho Aprili 7, mwaka huu walipoichapa 2-0 Welayta Dicha ya Ethiopia katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika wakiwa chini ya kocha wao, Mzambia George Lwandamina na tangu ameondoka leo wamefungwa mechi ya tano na kutoa sare nne.

  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Singida United wameichapa Maji Maji ya Songea mabao 3-2 Uwanja wa Namfua, Singida.
  Mabao ya Singida United yamefungwa na Deus Kaseke dakika ya 12, Shafiq Batambuze dakika ya 31 na  Tafadzwa Kutinyu dakika ya 36, wakati ya Maji Maji yamefungwa na Jerry Tegete dakika ya 62 na Jaffar Mohammed dakika ya 63.
  Lipuli FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Samora mjini Iringa, bao pekee la Mussa Nampaka ‘Chibwabwa’ dakika ya 76.
  Mjini Dar es Salaam, Uwanja wa Taifa bao pekee la Edward Christopher Shijja kwa kichwa dakika ya 84 akimalizia krosi ya Japhet Makalai kutoka upande wa kulia limeipa Kagera Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Simba SC Uwanja wa Taifa mjini Katika mchezo uliohudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk, John Pombe Joseph Magufuli.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YA SASA NI ‘KICHWA CHA MWENDAWAZIMU’…LEO IMEPIGWA 1-0 NA MWADUI SHINYANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top