• HABARI MPYA

  Wednesday, May 02, 2018

  TIMU ZA MAJESHI ZATAWALA LIGI KUU UNGUJA, PEMBA NI ZA URAIANI ZAIDI

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  TIMU za Majeshi tupu ndizo zipo kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kushiriki hatua ya Nane Bora ya Ligi Kuu ya Zanzibar msimu huu, ambayo hushirikisha pia na timu nne za Pemba.
  Hizo ni timu za Kikosi cha Valentia (KVZ), Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Mafunzo inayomilikiwa na Jeshi la Magereza, Polisi na Zimaamoto, ambayo ni timu ya Kikosi cha Zimamoto na Uokozi. 
  Hizo ndizo timu ambazo kwa sasa zipo kwenye nafasi tano za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Unguja zikiwania nafasi nne za kushiriki Ligi Kuu ya Zanzibar.
  KVZ inaongoza mbio hizo kwa pointi zake 46, ikifuatiwa na JKU pointi 42, Mafunzo 41 sawa na Polisi, wakati Zimamoto ina pointi 40 zote zikiwa zimecheza mechi 24 kuelekea mechi mbilimbiliza mwisho kwenye ligi ya timu 14.
  Mbali na timu ya kwanza hadi ya nne kufuzu kushiriki Super 8 ya Ligi Kuu ya Zanzibar, timu zitakazoshika nafasi ya tano hadi ya nane zitabaki Ligi Kuu ya Unguja, wakati timu zitakazoshika nafasi ya tisa hadi ya 14 zitaipa mkono wa kwaheri ligi hiyo msimu ujao.
  Timu zilizofuzu Nane Bora ya Ligi Kuu ya Zanzibar kutoka Pemba ni Mwenge, Jamhuri zilizoshiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi Januari mwaka huu, Opec iliyopanda msimu huu na Hard Rock, ambayo pia inamilikiwa na Jeshi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TIMU ZA MAJESHI ZATAWALA LIGI KUU UNGUJA, PEMBA NI ZA URAIANI ZAIDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top