• HABARI MPYA

  Wednesday, May 02, 2018

  LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KUANZA JUMAPILI IKISHIRIKISHA TIMU 28

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  LIGI ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Jumapili Mei 6 na kumalizika Mei 22,2018 kwenye vituo vinne.
  Ligi hiyo ya RCL itashirikisha timu 28 zilizogawanywa kwenye makundi manne kwenye vituo vya Geita, Singida, Rukwa na Kilimanjaro na kila kundi kwenye kituo likiwa na timu 7.
  Kila kundi litapandisha timu 2 wakati zitakazobaki zitarudi ligi ya mkoa.
  Kundi A linaundwa na timu za Gipco FC ya Geita, Ungindoni FC ya Dar es Salaam, Ambassador FC ya Shinyanga na Kumunyange FC ya Kagera na Zimamoto ya Shinyanga.
  Kundi B linaundwa na timu za Laela FC ya Rukwa, Tukuyu Stars ya Mbeya, Tabora FC ya Tabora, Migombani FC ya Songwe, Kasulu Red Star FC ya Kigoma, Black Belt ya Ruvuma na Watu FC ya Katavi.
  Kundi C linaundwa na timu za Stand Dortmund ya Singida, Temeke Squad ya Temeke, Mwena FC ya Mtwara, Kipagalo FC ya Njombe, Gwassa SC ya Dodoma, Maji Maji Rangers ya Lindi na Mtwivila City FC ya Iringa.
  Kundi D lina timu za Uzunguni FC ya Kilimanjaro, Karume Market ya Dar es Salaam, Usalama SC ya Manyara, Bishop Dsports ya Arusha, Moro Kids ya Morogoro, Stand FC ya Pwani na Sahare All Stars ya Tanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KUANZA JUMAPILI IKISHIRIKISHA TIMU 28 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top