• HABARI MPYA

  Wednesday, May 16, 2018

  SOUTHGATE AITA 23 WA MWISHO ENGLAND KOMBE LA DUNIA

  KOCHA Gareth Southgate ametaja kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 cha timu ya taifa ya England kilichosheheni wazoefu kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia.
  Ndani ya kikosi hicho, kocha huyo amemjumuisha beki mkongwe mwenye umri wa miaka 32, Gary Cahill wa Chelsea ambaye ameichezea mechi 58 timu hiyo.
  Southgate pia amewaita wote, Trent Alexander-Arnold na Kieran Trippier kwa ajlii ya beki ya kulia.
  Alexander-Arnold mwenye umri wa miaka 19, amechukuliwa kwenye kikosi hicho baada ya kazi nzuri akiwa na Liverpool kwenye michuano yote, Ligi Kuu ya England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Kati ya wachezaji aliowaita Southgate watano, Jordan Henderson, Raheem Sterling, Danny Welbeck, Phil Jones na Cahill walikuwepo kwenye fainali zilizopita za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil. 
  Hakuna kati yao amewahi kushinda mechi ya Kombe la Dunia.


  Trent Alexander-Arnold ni miongoni mwa wachezaji 23 walioitwa na kocha Gareth Southgate kwenye kikosi cha England kwa ajili ya kombe la Dunia PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  KIKOSI KAMILI CHA TIMU YA TAIFA YA ENGLAND;
  Makipa; Jordan Pickford (Everton), Jack Butland (Stoke), Nick Pope (Burnley)
  Mabeki; John Stones (Manchester City), Gary Cahill (Chelsea), Phil Jones (Manchester United), Harry Maguire (Leicester), Kyle Walker (Manchester City), Trent Alexander-Arnold (Liverpool), Ashley Young (Manchester United), Danny Rose (Tottenham), Kieran Trippier (Tottenham)
  Viungo; Eric Dier (Tottenham), Jordan Henderson (Liverpool), Dele Alli (Tottenham), Ruben Loftus-Cheek (Chelsea), Jesse Lingard (Manchester United), Raheem Sterling (Manchester City), Fabian Delph (Manchester City)
  Washambuliaji; Harry Kane (Tottenham), Jamie Vardy (Leicester), Danny Welbeck (Arsenal), Marcus Rashford (Manchester United)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SOUTHGATE AITA 23 WA MWISHO ENGLAND KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top