• HABARI MPYA

  Wednesday, May 16, 2018

  LIPULI YAILAMBA MTIBWA SUGAR 2-1 MANUNGU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Lipuli ya Iringa imeizima Mtibwa Sugar kwa kuichapa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
  Shujaa wa mchezo wa leo alikuwa ni kiungo mshambuliaji wa zamani wa Azam FC, Sefi Abdallah Karihe aliyefunga mabao yote mawili Lipuli dakika za 17 na 71, wakati la Riffat Khamisi dakika ya 53.  
  Ushindi huo unaifanya Lipuli FC ifikishe pointi 35 baada ya kucheza mechi 28, wakati Mtibwa Sugar inafikisha pointi 37 baada ya kucheza mechi 28.

  Ligi Kuu itaendelea Ijumaa kwa mechi mbili, Njombe Mji FC wakiikaribisha Mtibwa Sugar Uwanja Saba Saba mjini Njombe na Stand United wakiwa wenyeji wa Mbao FC Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
  Jumamosi kutakuwa na mechi tatu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Simba wataikaribisha Kagera Sugar na Azam Complex, Chamazi, Azam FC wataikaribisha Tanzania Prisons, wakati Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga  Mwadui watakuwa wenyeji wa Yanga.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIPULI YAILAMBA MTIBWA SUGAR 2-1 MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top