• HABARI MPYA

    Friday, May 11, 2018

    SAMATTA ATOKEA BENCHI NA KUMALIZA UKAME WA MABAO WA ZAIDI YA NUSU MWAKA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa Alhamisi ametokea benchi na kuifungia bao la kusawazisha KRC Genk ikipata sare ya 1-1 na AA Gent katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
    Samatta aliingia uwanjani dakika ya 54 kwenda kuchukua nafasi ya mshambuliaji Mgiriki, Nikolaos Karelis wakati huo tayari Gent wanaongoza kwa 1-0, bao lililofungwa na mshambuliaji kutoka Japan, Yuya Kubo dakika ya 15 akimalizia kazi nzuri ya kiungo kutoka Georgia, Giorgi Chakvetadze.
    Samatta alifunga bao lake dakika ya 66, ambalo linakuwa la kwanza tangu Oktoba 25, mwaka jana alipofunga bao la pili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Club Brugge katika Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji, Uwanja wa Luminus Arena pia.
    Mbwana Samatta akikimbia kushangilia baada ya kuifungia bao la kusawazisha KRC Genk
    Samatta, mshambuliaji wa zamani wa Mbagala Market, African Lyon na Simba za Tanzania leo amefunga bao lake la 23 katika mechi ya 87 tangu Nahodha huyo wa Taifa Stars ajiunge na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). 
    Kikosi chs KRC Genk; Vukovic, Nastic, Colley, Aidoo/Dewaest dk88, Mata, Seck, Malinovskyi, Pozuelo, Trossard, Ndongala/Wouters dk53 na Karelis/Samatta dk53.
    AA Gent : Kalinic, Gigot, Rosted, Verstraete, Chakvetadze (32 'Kalu) (69' Janga), Yaremchuk, Dejaegere, Asare, Bronn, Simon and Kubo (78 'Esiti).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA ATOKEA BENCHI NA KUMALIZA UKAME WA MABAO WA ZAIDI YA NUSU MWAKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top