• HABARI MPYA

  Saturday, May 12, 2018

  PAMOJA NA KUFUNGWA, TIMU YA BANDA YANUSURIKA KUSHUKA DARAJA AFRIKA KUSINI

  Na Mwandishi Wetu, PRETORIA
  BEKI wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Hassan Banda ataendelea kucheza Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini msimu ujao pamoja na timu yake, Baroka FC kuchapwa bao 1-0 na SuperSport United katika mchezo wake wa mwisho wa ligi hiyo Uwanja wa Lucas Masterpieces Moripe mjini Pretoria.
  Mbabe wa mechi ya leo ni beki Muafrika Kusini mwenye umri wa miaka 22, Maphosa Modiba aliyefunga bao pekee kwa penalti dakika ya 26.
  Matokeo hayo yanaifanya SuperSport ifikishe pointi 36 baada ya kucheza mechi zote 30 za PSL msimu huu na kupanda hadi nafasi ya 11 kutoka ya 13, huku Baroka sasa ikiwa ya mwisho baada ya timu mbili, Platinum Stars na Ajax Cape Town kuteremka.
  Abdi Banda ataendelea kucheza Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini msimu ujao pamoja na Baroka FC kuchapwa bao 1-0 na SuperSport United leo

  Baroka inabaki na pointi zake 34 za mechi 30, wakati Platinum Stars inateremka daraja huku Ajax Cape Town ikienda kucheza Ligi ndogo dhidi ya timu iliyoshika nafasi ya pili na ya tatu katika Ligi Daraja la Kwanza ili kuwania kupanda tena Ligi Kuu.
  Mamelodi Sundowns ndiyo mabingwa wa ABSA msimu huu kwa pointi zao 60 baada ya mechi 30, wakiipiku Orlando Pirates iliyomaliza na poini 55 huku waliokuwa mabingwa watetezi, Bidvest Wits wakimaliza nafasi ya 12 kwa pointi zao 36.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PAMOJA NA KUFUNGWA, TIMU YA BANDA YANUSURIKA KUSHUKA DARAJA AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top