• HABARI MPYA

  Saturday, May 19, 2018

  MTIBWA SUGAR YAWAIBUKIA NJOMBE MJI KIKAMILIFU

  Na Mwandishi Wetu, NJOMBE
  TIMU ya Mtibwa Sugar SC ya Turiani mkoani Morogoro imewasili mjini Njombe jana ikiwa na kikois chake kamili kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Njombe Mji FC kesho Uwanja wa Saba Saba.
  Wachezaji waliowasili na Mtibwa Sugar kwa ajili ya mchezo huo ni makipa Shaaban Hassan Kado na Aden Salvatory ambaye anatumikia kikosi cha timu ya vijana ya Mtibwa Sugar.
  Mabeki ni Rodgers Gabriel, Issa Rashid 'Baba Ubaya', Hassan Isihaka, Cassian Ponera 'Pepe' na Dickson Daudi Mbeikya.
  Viungo ni Saleh Khamis Abdallah, Hassan Dilunga, Shaaban Mussa Nditi, Onesmo Mpakama Mayaya, Ayoub Semtawa na Ally Makarani.

  Washambuliaji ni Riffat Khamis Msuya, Joseph Mkua Mkele 'Jojo', Haruna Chanongo, Salum Kihimbwa na  Nassoro Ally Kiziwa.
  Mchezo huo wa Jumapili utakuwa mkali na wa kipekee kutokana na timu hizo kila mmoja kuitaji pointi tatu muhimu Mtibwa Sugar wanaitaji kushika nafasi za juu zaidi hivyo wanataka kushinda mchezo huo huku upande wa Njombe Mji wakipambana kuepuka kushuka daraja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAWAIBUKIA NJOMBE MJI KIKAMILIFU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top