• HABARI MPYA

  Monday, May 14, 2018

  KICHUYA JANA KAPIGA BAO SIMBA IKITOKA SARE YA 2-2 NA WATOTO WA DODOMA…WAZIRI MKUU DK MAJALIWA ALIKUWA JUKWAANI

  Na Mwandishi Wetu, DODOMA
  SIMBA SC jana ililazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Kombaini ya Dodoma katika mchezo wa kirafiki uliohudhuriwa na Waziri Mkuu, Dk. Kassim Majaliwa Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
  Simba ilianza kuandika bao kunako dakika ya 29 kupitia kwa mshambuliaji wake, Shiza Kichuya kwa njia ya Penalti.
  Penalti hiyo ilitolewa na mwamuzi Salum Mambo mara baada ya kiungo Mohammed Ibrahim kuchezewa faulo na beki wa kati wa Dodoma Combine, Ibrahim Ngecha.
  Simba iliandika bao la pili kunako dakika ya 44 kupitia kwa beki wake wa kulia, Shomari Ally na hadi mapumziko Simba walikuwa mbele kwa mabao 2-0.
  Kipindi cha pili Dodoma Combine walikianza kwa kasi na kufanikiwa kupata bao kunako dakika 49 lilofungwa na mshambuliaji Anwar Jabir, aliyefunga kwa kichwa akimalizia krosi ya beki wa kulia, Nassor Masoud ‘Chollo’.
  Shiza Kichuya jana aliifungia Simba bao katika sare ya 2-2 na Dodoma Combine

  Simba ambayo katika mchezo wa jana ilichezesha wachezaji wengi wa kikosi cha pili huku wachezaji wa kikosi cha kwanza wakiwa jukwaani wakishihudia mtanange huo, pia benchi la ufundi liliongozwa na Kocha Msaidizi Mrundi, Masoud Juma huku Kocha Mkuu, Mfaransa Pierre Lechantre akiwa jukwaani wakati Dodoma FC ilikuwa chini ya kocha Jamhuri Kihwelo.
  Mgeni rasmi katika mchezo huo alikuwa Waziri Mkuu, Dk. Kassim Majaliwa na aliongozana na Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Mwijage na Wabunge wengine.
  Kikosi cha Dodoma Combine kilikuwa; Leonard Mkinga, Nassor Masoud ‘Chollo’, Anderson Solomon, Salim Materazi, Ibrahim Ngecha, Razak Khalfan, Samir Ringo, Jeremiah Haule/Abas Kapombe dk72, Anwar Jabir, Daudi Augustine, Ibrahim Mbogamasoli.
  Simba SC: Said Mohammed ‘Nduda’, Ally Shomari, Jamal Mwambeleko, Kevin Faru, Vincent Costa, Said Ndemla, Mohammed Ibrahim ‘Mo’, Haruna Niyonzima, Rashid Juma, Shiza Kichuya na Muzamir Yassin.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KICHUYA JANA KAPIGA BAO SIMBA IKITOKA SARE YA 2-2 NA WATOTO WA DODOMA…WAZIRI MKUU DK MAJALIWA ALIKUWA JUKWAANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top