• HABARI MPYA

  Monday, May 21, 2018

  HISPANIA YATAJA KIKOSI CHA MWISHO CHA KOMBE LA DUNIA

  Kipa wa Manchester United, David De Gea ndiye mlinda mlango namba moja wa Hispania kuelekea Kombe la Dunia Urusi PICHA ZAIDI GONGA HAPA  


  KIKOSI CHA WACHEZAJI 23 WA HISPANIA KOMBE LA DUNIA 

  Makipa: Kepa Arrizabalaga, David De Gea, Pepe Reina
  Mabeki: Dani Carjaval, Alvaro Odriozola, Sergio Ramos, Jordi Alba, Gerard Pique, Nacho, Nacho Monreal, Cesar Azpilicueta
  Viungo: Sergio Busquets, Saul Niguez, Koke, Thiago Alcantara, Andres Iniesta, David Silva, Isco, Marco Asensio, Lucas Vazquez
  Forwards: Iago Aspas, Rodrigo Moreno, Diego Costa
  TIMU ya taifa ya Hispania imetaja wachezaji 23 kwa ajili ya kikosi cha Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 huku kocha Julen Lopetegui akimtema mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata.
  Nyota wa Ligi Kuu ya EnglandDavid De Gea, David Silva, Cesar Azpilicueta na Nacho Monreal wote wamejumuishwa kwenye kikosi hicho pamoja na kiungo anayeondoka Barcelona, Andres Iniesta. 
  Wakongwe, Gerard Pique, Sergio Ramos, Jordi Alba na Sergio Busquets wote wameitwa huku Diego Costa akipewa pia nafasi kwenye ndege ya kwenda Urusi.
  Nyota wa zamani wa Liverpool, Iago Aspas na Rodrigo Moreno wa Valencia wameitwa pia katika safu ya ushambuliaji ya Hispanhia badala ya Morata na watagombea nafasi na Diego Costa.
  Wachezaji wengine maarufu waliotemwa ni pamoja wachezaji wenzake Morata wa Chelsea, Cesc Fabregas, Marcos Alonso, Hector Bellerin wa Arsenal na kiungo wa Atletico Madrid, Vitolo. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HISPANIA YATAJA KIKOSI CHA MWISHO CHA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top