• HABARI MPYA

  Tuesday, May 01, 2018

  SERENGETI BOYS WAWASILI DAR NA KOMBE LAO LA CECAFA U17, WAPOKEWA NA WAZIRI MWAKYEMBE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imerejea nchini Alfajiri ya leo kutoka Bujumbura, Burundi ambako Jumapili ilifanikitwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge U-17 kwa ushindi 2-0 dhidi ya Somalia Uwanja wa Ngozi.
  Ushindi huo ulitokana na mabao ya Edson Jeremiah dakika ya 25 na Jaffar Mtoo dakika ta 66 katika mchezo ambao Serengeti Boys ilionyesha kiwango cha hali ya juu na kuwafurahisha mashabiki.
  Ikumbukwe Somalia imefika hatua hii baada ya kuwatoa Uganda, wakati Tanzania iliwatoa Kenya katika mechi za Nusu Fainali. 

  Awali, Serengeti Boys ilikuwa iwasili Alfajiri ya kesho, lakini Baraza la Vyama na Klabu za Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) likawabadilishia tiketi za ndege mabingwa hao wawahi kurejea nyumbani.
  Msafara wa Serengeti Boys ulioongozwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), umepokewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembem ambaye amewapongeza vijana kwa ushindi huo.
  Katika mashindano hayo, Serengeti Boys iliyo chini ya Mshauri wa Ufundi, Mdenmark Kim Poulsen na Kocha Oscar Milambo na Peter Manyika anayewanoa makipa, ilitoka sare ya 1-1 na Uganda kabla ya kuifunga Sudan 6-0 kwenye Kundi lake, B na baadaye kuichapa Kenya mabao 2-1 kwenye Nusu fainali na kushinda mabao 2-0 dhidi ya Somalia kwenye fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS WAWASILI DAR NA KOMBE LAO LA CECAFA U17, WAPOKEWA NA WAZIRI MWAKYEMBE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top