• HABARI MPYA

  Tuesday, May 01, 2018

  SAMATTA AWAPONGEZA SERENGETI BOYS NA KUWAAMBIA; “MSIKIMBILIE KUOA”

  Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Ally Samatta amewapongeza taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge U-17 nchini Burundi.
  Serengeti Boys Jumapili ilifanikitwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge U-17 baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Somalia, mabao ya Edson Jeremiah dakika ya 25 na Jaffar Mtoo dakika ta 66 Uwanja wa Ngozi, Bujumbura.
  Mbwana Samatta amewapongeza Serengeti Boys kwa kutwaa ubingwa CECAFA Challenge U-17 nchini Burundi

  Na leo Nahidha wa Taifa Stars ameposti katika akaunti yake ya twitter akiwapongeza na kuwatania kidogo; “Hongereni sana 'Serengeti' (u17) kwa ubingwa wa cecafa kwa umri wa chini ya miaka 17. Tunamini TFF ina mipango mikubwa juu yenu. Tulizeni vichwa madogo, tusianze kusikia mmeanza kuoa sasa (utani). Hongereni sana,”.
  Serengeti Boys imerejea nchini Alfajiri ya leo na kupokewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembem ambaye amewapongeza vijana kwa ushindi huo.
  Katika mashindano hayo, Serengeti Boys iliyo chini ya Mshauri wa Ufundi, Mdenmark Kim Poulsen na Kocha Oscar Milambo na Peter Manyika anayewanoa makipa, ilitoka sare ya 1-1 na Uganda kabla ya kuifunga Sudan 6-0 kwenye Kundi lake, B na baadaye kuichapa Kenya mabao 2-1 kwenye Nusu fainali na kushinda mabao 2-0 dhidi ya Somalia kwenye fainali.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AWAPONGEZA SERENGETI BOYS NA KUWAAMBIA; “MSIKIMBILIE KUOA” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top