• HABARI MPYA

  Tuesday, May 01, 2018

  MWADUI FC YATAKA KUENDELEZA WIMBI LA USHINDI BAADA YA KUIPIGA MBAO JANA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa Mwadui FC, Paul Nonga amesema kwamba wanataka kushinda mechi zao zote zilizosalia za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ili kumaliza katika nafasi nzuri zaidi.
  Nonga ameyasema hayo baada ya ushindi wa 1-0 jana dhidi ya Mbao FC ya Mwanza Uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga.
  "Tumefurahi sana kwa ushindi huu wa nyumbani kwa sababu unatuongezea pointi ambazo zitatusaidia kumaliza katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu,"amesema Nonga, mshambuliaji wa zamani wa Yanga.

  Kwa ushindi huo uliotokana na bao la Charles Ilanya Mwadui FC sasa inafikisha pointi 29 na kupanda hadi nafasi ya tisa kutoka ya 12 na kuzishusha Kagera Sugar yenye pointi 27, Mbeya City pointi 28 na Stand United pointi 29. 
  Mbao FC inabaki nafasi ya 13 kwa pointi zake 26 baada ya kucheza mechi 26.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWADUI FC YATAKA KUENDELEZA WIMBI LA USHINDI BAADA YA KUIPIGA MBAO JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top