• HABARI MPYA

  Sunday, May 13, 2018

  SALAH ABEBA KIATU CHA DHAHABU ENGLAND, LIVERPOOL YAUA 4-0

  Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah akiwa ameshika kiatu cha dhahabu baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Brighton & Hove Albion leo Uwanja wa Anfield alichokabidhiwa kufuatia kuibuka mfungaji bora wa ligi hiyo kwa mabao yake 32 la mwisho akifunga leo dakika ya 26 katika ushindi wa 4-0, mabao mengine yamefungwa na Dejan Lovren dakika ya 40, Dominic Solanke dakika ya 53 na Andy Robertson dakika ya 85.
  Salah amempiku Harry Kane wa Tottenham Hotspur aliyemaliza na mabao 30, huku Liverpool ikipanda hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 77, nyuma ya Toottenham pointi 77, Manchester United pointi 81 na Manchester City 100 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SALAH ABEBA KIATU CHA DHAHABU ENGLAND, LIVERPOOL YAUA 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top