• HABARI MPYA

  Saturday, May 12, 2018

  MSAIDIZI WA MOURINHO KWA MIAKA 17 AACHIA NGAZI MAN UNITED

  Rui Faria, Msaidizi muaminifu wa muda mrefu wa Jose Mourinho ataondoka Manchester United mwishoni mwa PICHA ZAIDI GONGA HAPA  


  MIAKA 17 YA RUI FARIA KUWA MSAIDIZI WA JOSE MOURINHO

  Leiria (2001-02)
  Porto (2002-04)
  Chelsea (2004-07 & 2013-15)
  Inter Milan (2008-10)
  Real Madrid (2010-13)
  Manchester United (2016-18)
  MATAJI
  Porto 
  Liga Ureno(200-2-03 and 2003-04)
  Kombe la Ureno (2002-03)
  Super Cup ya Ureno (2002-03) 
  Kombe la UEFA (2002-03)
  Ligi ya Mabingwa (2003-04)
  Chelsea
  Ligi Kuu England (2004-05, 2005-06 and 2014-15)
  Kombe la FA (2006-07)
  Kombe la Ligi (2004-05, 2005-06 and 2014-15)
  Ngao ya Jamii (2004-05)
  Inter Milan
  Serie A (2008-09 na 2009-10)
  Kombe la Italia (2009-10)
  Super Cup ya Italia (2008-09) 
  Ligi ya Mabingwa (2009-10)
  Real Madrid
  La Liga (2011-12)
  Spanish Cup (2010-11)
  Spanish Super Cup (2012-13)
  Manchester United
  Ngao ya Jamii (2016-17)
  Kombe la Ligi (2016-17)
  Europa League (2016-17) 
  KOCHA Rui Faria, Msaidizi muaminifu wa muda mrefu wa Jose Mourinho ataondoka Manchester United mwishoni mwa msimu.
  Kijana huyo wa umri wa miaka 42, ambaye alikuwa anahusishwa na ukocha wa Arsenal, nafasi iliyo wazi anataka kutumia muda zaidi na familia kabla ya kujipima kufanya kazi peke yake na amendoka kwa baraka za Mourinho.
  Faria amefanya kazi na Mourinho kwa miaka 17 na kuondoka kwake kutaibua maswali, nani atarithi nafasi yake huku Nahodha wa klabu, Michael Carrick anapewa nafasi zaidi. 
  Faria alikuwa miongoni mwa makocha watatu ambao Mourinho aliwaamini alioingia nao England kwa mara ya kwanza kufundisha Chelsea mwaka 2004.
  Na hiyo ni baada ya awali kufanya kazi na Mourinho alipokuwa Msaidizi wa Luis Van Gaal klabu ya Barcelona. 
  Faria baada ya kupata Shahada ya Elimu ya Utimamu wa Mwili maalum kwa makocha alikwenda kwenye semina Nou Camp ambako ndiko alikutana na Mourinho. 
  Mourinho alivutiwa na Faria kwa ujumla kutokana na upeo wake katika mchezo na falsafa zake pia ambazo ziliendana na zake. 
  Kisha Faria ambaye wakati huo alikuwa ana umri wa miaka 25 akapewa kazi na Mourinho kuwa Msaidizi wake alipokuwa katika timu ndogo tu ya Leiria ya Ureno mwaka 2001.
  Mpango wake wa kwanza ni kuwa kocha wa mazoezi ya utimamu wa mwili na mchambuzi wa video, lakini akatokea kuwa mtu muhimu kwa Mourinho.
  Katika miaka yao 17 ya kufanya kazi pamoja, wameshinda mataji manne makubwa ya Ulaya yakiwemo ya Kombe la UEFA na Ligi ya Mabingwa Ulaya mfululizo wakiwa na Porto ambayo yalikuza soko la Mourinho kwenye ramani ya soka. Pia wameshinda mataji ya La Liga na Serie A, matatu ya Ligi Kuu England na tisa ya vikombe vya nchi mbalimbali.
  Mechi ya mwisho ya Faria kama Msaidizi wa Mourinho ndani ya Man United itakuwa wiki ijayo katika fainali ya Kombe la FA dhidi ya timu yao ya zamani, Chelsea.
  Mechi ya nyumbani dhidi ya Watford kesho itampa nafasi Faria kuwaaga mashabiki wa Man United Uwanja wa Old Trafford.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSAIDIZI WA MOURINHO KWA MIAKA 17 AACHIA NGAZI MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top