• HABARI MPYA

    Wednesday, May 02, 2018

    MAREFA WA GHANA NA NIGERIA KUCHEZESHA MECHI YA YANGA NA U.S.M. ALGRER JUMAPILI ALGIERS

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    REFA Daniel Nii Ayi Laryea wa Ghana ndiye atachezesha mechi ya ufunguzi ya hatua ya 16 Bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji, U.S.M Alger na Yanga SC ya Tanzania Jumapili Uwanja wa Julai 5 mjini Algiers, Algeria.
    Pamoja na Laryea, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limewateua Abel Baba wa Nigeria na David Laryea wa Ghana pia kuwa waamuzi wasaidizi, maarufu kama washika vibendera katika mchezo huo wa Kundi D uliopangwa kuanza Saa 2:00 usiku na Saa 4:00 usiku kwa saa za Tanzania.
    Yanga Sc inatarajiwa kuondoka nchini kesho kwenda Algiers kwa ndege ya Emirates Air ikipitia Dubai tayari kwa mchezo huo wa kwanza wa Kundi D Kombe la Shirikisho la Soka Afrika dhidi ya U.S.M. Alger Jumapili.
    Pamoja na Yanga na USM Alger, timu nyingine katika Kundi D ni Rayon Sport ya Rwanda na Gor Mahia ya Kenya ambazo zitamenyana zenyewe katika ufunguzi wa hatua ya 16 Bora ya Kombe Shirikisho Afrika.
    Ikumbukwe Kundi A lina timu za ASEC Mimosa ya Ivory Coast, Raja Club Athletic, maarufu Raja Casablanca ya Morocco, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Aduana Stars ya Ghana.
    Kundi B linaundwa na RS Berkane ya Morocco, Al Masry ya Misri, UD Songo ya Msumbiji na El Hilal ya Sudan, wakati Kundi C lina timu za CARA ya Kongo, Enyimba ya Nigeria, Williamsville na Djoliba ya Mali.
    Baada ya mechi ya kwanza ugenini Jumapili, Yanga itamenyana na Rayon Sport mjini Dar es Salaam Mei 16 na itakamilisha mechi za mzunguko wa kwanza kwa kuwafuata Gor Mahia mjini Nairobi Julai 18.
    Mzunguko wa pili Yanga itaanzia nyumbani Julai 29 na Gor Mahia, kabla ya kuwakaribisha na USMA Alger Agosti 19 na kwenda kumalizia ugenini Agosti 29 na Rayon.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAREFA WA GHANA NA NIGERIA KUCHEZESHA MECHI YA YANGA NA U.S.M. ALGRER JUMAPILI ALGIERS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top