• HABARI MPYA

  Wednesday, May 02, 2018

  DE GEA AWA MCHEZAJI BORA WA MWAKA MANCHESTER UNITED

  Kipa David de Gea akiwa ameshika tuzo yake ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Manchester United baada ya kukabidhiwa jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA 


  TUZO ZA MAN UNITED MSIMU WA 2017-18 

  Sir Matt Busby Mchezaji Bora wa Mwaka (chaguo la mashabiki) — David de Gea
  Mchezaji Bora wa Mwaka — David de Gea
  Meneja wa Wachezaji wa Mwaka — Scott McTominay
  Bao Bora la Msimu — Nemanja Matic (vs Crystal Palace)
  Mchezaji wa Timu ya Wachezaji wa Akiba ya Denzil Haroun wa Mwaka— Demetri Mitchell
  Mchezaji Bora wa Timu ya Vijana ya Jimmy Murphy wa Mwaka — Tahith Chong
  Tuzo Maalum— Michael Carrick
  KIPA Mspaniola, David de Gea ameshinda tuzo mbili katika sherehe za mwisho wa msimu za Manchester United usiku wa jana.
  Mlinda mlango huyo ambaye amedaka kila mechi ya Ligi Kuu ya England kwa muda wote msimu huu hadi sasa.
  Katika mechi 35 alizodaka hadi sasa, De Gea hakuruhusu bao hata moja katika mechi 17 kati ya hizo, hivyo kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kabla ya kubeba na tuzo ya Sir Matt Busby ya Mchezaji Bora wa Mwaka chaguo la mashabiki.
  Katika sherehe za jana ilishuhudiwa wachezaji wakifika na wake na mahawara zao, maarufu kama WAG ukumbi wa Uwanja wa Old Trafford. 
  De Gea alifika na mpenzi wake, nyota wa Pop, Edurne Garcia, ambaye aliiwakilisha Hispania katika shindano la kuimba wimbo Ulaya, lililojulikana kama Eurovision Song Contest mwaka 2015. 
  Mspaniola mwenzake, Juan Mata alifika na mkewe Evelina Kamph, wakati Ander Herrera alikwenda na mpenzi wake, Isabel Collado na Marcos Rojo alifika na mpenzi wake, Eugenia Lusardo.
  Nemanja Matic alisjhinda tuzo ya Bao Bora la msimu kutokana na bao lake la dakika za mwishoni alilofunga katika ushindi wa United wa 3-2 dhidi ya Crystal Palace mwezi Machi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DE GEA AWA MCHEZAJI BORA WA MWAKA MANCHESTER UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top