• HABARI MPYA

  Tuesday, May 15, 2018

  WASAIDIZI WOTE WA WENGER NAO WATIMULIWA ARSENAL

  WATU sita wa muda mrefu katika benchi la Ufundi la Arsenal wameondolewa – wakimfuata aliuekuwa bosi wao, Mfaransa Arsene Wenger.
  Klabu inajiandaa kwa zama mpya kabisa baada ya kuondoka kwa Arsene Wenger aliyedumu kwa miaka 22 na Mkuu wa Idara ya Tiba, Colin Lewin pamoja na makocha wasadizi Neil Banfield, Gerry Peyton, Tony Colbert na Paul Johnson wote wameondolewa.
  Wanaopewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi ya Wenger ni wachezaji wa zamani wa klabu hiyo, Mikel Arteta ambaye kwa sasa ni Msaidizi wa Pep Guardiola pale Manchester City, Patrick Vieira, ambaye kwa sasa ni kocha wa New York City, Julian Nagelsmann, ambaye kwa sasa anafundisha Hoffenheim anaeongoza mbio.
  Neil Banfield (kulia) ni mmoja watu waliokuwa wanafanya kazi na Arsene Wenger anayeondoka PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Inaelezwa kwa sababu za kifedha, klabu imeachana na mpango wa kuwafukuzia Luis Enrique na Massimiliano Allegri. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WASAIDIZI WOTE WA WENGER NAO WATIMULIWA ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top