• HABARI MPYA

  Monday, May 14, 2018

  RUVU SHOOTING YAENDELEA KUPAPASA WAPINZANI…YAWAGONGA 1-0 STAND UNITED

  BAO pekee la beki Rajab Zahir dakika ya 73 jioni ya leo Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani limetosha kuipa Ruvu Shooting ushindi wa 1-0 dhidi ya Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania  Bara.
  Ushindi huo unaifanya Ruvu Shooting kufikisha pointi 36 baada ya kucheza mechi 28, ingawa inaendelea kubaki nafasi ya saba, nyuma ya Mtibwa Sugar yenye pointi 37 za mechi 27.
  Ligi Kuu itaendelea kesho kwa mchezo mmoja, Mtibwa Sugar FC wakiikaribisha Lipuli FC Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RUVU SHOOTING YAENDELEA KUPAPASA WAPINZANI…YAWAGONGA 1-0 STAND UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top