• HABARI MPYA

    Wednesday, May 16, 2018

    KILA LA HERI YANGA SC, WAPIGENI HAO RAYON MFUFUE MATUMAINI YA ROBO FAINALI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    YANGA SC inateremka Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam Saa 1:00 usiku wa leo kumenyana na Rayon Sport ya Rwanda ktika mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika.
    Katika mchezo huo, Yanga SC watamkosa kiungo wao, Said Juma ‘Makapu’ ambaye atakuwa anatumikia adhabu ya kadi za njano.  
    Mechi hiyo itachezeshwa na maarefa kutoka Angola, Helder Martins De Carvalho atakayepulisza filimbi akisaidiwa na washika vibendera Ivanildo Meirelles De O Sanche Lopes na Wilson Valdmiro Ntyamba na viingilio ni Sh. 15,000 kwa VIP A, 7,000 kwa VIP B na C na 3,000 kwa mzunguko.
    Yanga itaingia kwenye mechi hiyo ikitoka kucheza mechi saba bila ya ushindi, tangu waliposhinda Aprili 7, mwaka huu walipoichapa 2-0 Welayta Dicha ya Ethiopia katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika wakiwa chini ya kocha wao, Mzambia George Lwandamina.
    Baada ya mchezo huo, Lwandamina alipakia mizigo yake kurejea kwao na tangu hapo Yanga hawajashinda tena, katika mechi saba, wakifungwa tano na kutoa sare mbili.
    Yanga ilianza vibaya mechi za makundi Kombe la Shirikisho Mei 6 kwa kufungwa mabao 4-0 na wenyeji, U.S.M. Alger Uwanja wa Julai 5, 1962 mjini Algiers, Algeria wakati Rayon ililazimishwa sare ya 1-1 na Gor Mahia siku hiyo mjini Kigali.
    Michuano ya Kombe la Shirikisho itasimama baada ya mechi za katikati ya wiki hii, Yanga na Rayon na Gor Mahia na USM Alger kupisha Fainali za kombe la Dunia mwezi ujao nchini Urusi. Yanga watakamilisha mechi zao za mzunguko wa kwanza kwa kuwafuata Gor Mahia mjini Nairobi Julai 18.
    Mzunguko wa pili Yanga itaanzia nyumbani Julai 29 na Gor Mahia, kabla ya kuwakaribisha na USMA Alger Agosti 19 na kwenda kumalizia ugenini Agosti 29 na Rayon.
    Timu mbili za juu kutoka kila kundi katika makundi yote manne, zitakutana katika hatua ya Robo Fainali na baadaye Nusu Fainali itakayozaa Fainali. Kila la heri Yanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KILA LA HERI YANGA SC, WAPIGENI HAO RAYON MFUFUE MATUMAINI YA ROBO FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top