• HABARI MPYA

  Tuesday, July 24, 2012

  TADDY, ADEBAYOR WANOGESHA VITA YA KIATU CHA DHAHABU KAGAME


  Taddy wa AS Vita, Azam wachunge sana huyu mtu

  Na Prince Akbar
  VITA ya kuwania kiatu cha dhahabu cha Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame imezidi kupambana moto, baada ya Taddy Etikiama kumpita Said Bahanuzi ‘Spider Man’ wa Yanga kwa bao moja, kufuatia kufunga kwenye Robo Fainali dhidi ya Atletico ya Burundi leo.
  Taddy sasa ana mabao sita, akifuatiwa na Spider Man mwenye mabao matano, wakati Hamisi Kiiza ‘Diego’hayuko mbali nao sana, akiwa ana mabao manne, sawa na John Bocco ‘Adebayor’ wa Azam FC.
  Wachezaji wote hao wanne timu zao zimeingia Nusu Fainali na wana nafasi ya kuongeza mabao yao, kwani wana mechi mbili zaidi kila mmoja kuelekea kipyenga cha kuhitimisha Kagame ya 2012.
  Wengine waliomo kwenye kinyang’aniyo hicho ni Suleiman Ndikumana wa APR mwenye mabao mabao matatu, wakati Abdallah Juma ‘Dullah Mabao’ wa Simba SC timu yake imetolewa leo akiwa ana mabao mawili sawa na Leonel St Preus wa APR, Didier Kavumbagu wa Atletico, Feni Ali na Robert Ssentongo wa URA.

  WANAOONGOZA KWA MABAO:
  Taddy Etikiama                 AS Vita         6
  Said Bahanuzi                   Yanga SC     5
  Hamisi Kiiza                      Yanga SC     4
  John Bocco                        Azam FC      4
  Suleiman Ndikumana       APR              3
  Abdallah Juma                  Simba SC     2
  Leonel St Preus                 APR              2
  Didier Kavumbagu            Atletico         2
  Feni Ali                               URA              2
  Robert Ssentongo             URA              2 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TADDY, ADEBAYOR WANOGESHA VITA YA KIATU CHA DHAHABU KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top