• HABARI MPYA

  Monday, July 23, 2012

  SPIDER MAN AONGOZA KWA MABAO KAGAME


  Spider Man; Bahanuzi

  Na Prince Akbar
  MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Said Bahanuzi ‘Spider Man’ anachuana vikali na mshambuliaji wa AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu kwenye michuano ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
  Bahanuzi, aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar msimu huu, ana mabao matano hadi sasa na mpinzani wake ana matano pia, lakini moja alifunga kwa penalti kwenye mechi dhidi ya Simba SC.
  Ina maana, kama mwendo utakuwa huu hadi mwisho wa siku wachezaji hao kufungana kwa mabao, basi Bahanuzi atapewa kiatu cha dhahabu kwa sababu hana bao la penalti, zaidi ya alilofunga lao kwenye mechi dhidi ya Mafunzo katika penalti za kuamua mshindi baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90, ambalo halijaingizwa kwenye orodha ya mabao yake.
  Hamisi Kiiza ‘Diego’, nyota mwingine wa Yanga kutoka Uganda, anashika nafasi ya pili kwa mabao yake manne, akifuatiwa na Suleiman Ndikumana wa APR matatu, Abdallah Juma ‘Dullah Mabao’ wa Simba SC, Leonel St Preus wa APR, Didier Kavumbagu wa Atletico, Feni Ali na Robert Ssentongo wa URA, wote mabao mawili kila mmoja.

  WANAOONGOZA KWA MABAO:
  Taddy Etikiama                AS Vita       5
  Said Bahanuzi                  Yanga SC   5
  Hamisi Kiiza                     Yanga SC   4
  Suleiman Ndikumana      APR             3
  Abdallah Juma                 Simba SC   2
  Leonel St Preus               APR             2
  Didier Kavumbagu          Atletico        2
  Feni Ali                             URA             2
  Robert Ssentongo           URA             2 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SPIDER MAN AONGOZA KWA MABAO KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top