• HABARI MPYA

  Friday, July 20, 2012

  URA WAIPELEKA SIMBA ROBO FAINALI KAGAME


  Simba SC

  Na Prince Akbar
  RASMI Simba SC imetinga Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya URA ya Uganda kuifunga Ports ya Djibouti, mabao 3-1, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Ports sasa imeaga na Simba imekuwa moja ya timu tatu zilizoingia Robo Fainali kutoka Kundi hilo na itaingia kwenye mchezo wa kesho dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kutafuta kupanda kutoka kutoka nafasi ya tatu ilipo sasa.
  Mabao ya URA katika mchezo wa leo, yalitiwa kimiaini na Augustine Nsumba dakika ya 23, Sam Mubiru dakika ya 38 na Robert Ssentongo dakika ya 56, wakati la kufutia machozi la Ports lilifungwa na Roland Ayuk Agbor dakika ya 68.
  Kwa matokeo hayo, URA inaendelea kuongoza Kundi A, kwa pointi zake tisa, baada ya kushinda mechi zake zote tatu na AS Vita inashika nafasi ya pili, wakati
  mabingwa wa Tanzania, Simba SC wanashika nafasi ya tatu, kwa pointi zao tatu baada ya kucheza mechi mbili, kufungwa moja na kushinda moja.
  Kazi ngumu iko Kundi B, baada ya jana Tusker ya Kenya, kutoka sare ya bila kufungana na Mafunzo ya Zanzibar.
  Sasa kundi hilo, ambalo kuna Azam FC pia limezidi kuwa gumu na kesho Tusker na Azam FC zitakamilisha mechi za kundi hilo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, katika mchezo ambao timu itakayoshinda moja kwa moja itaungana na Mafunzo kutinga Robo Fainali.
  Hatima ya Mafunzo kucheza au kutocheza Robo Fainali inashikiliwa na mechi hiyo, kwani iwapo timu hizo zitatoka sare ya kuanzia mabao 2-2 zitakwenda zote Nane Bora na wawakilishi wa Zanzibar watarejea nyumbani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: URA WAIPELEKA SIMBA ROBO FAINALI KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top