• HABARI MPYA

  Saturday, July 21, 2012

  CHUNGA SANA JEZI 11 SIMBA NA YANGA

  11 ya Simba SC anavaa Dullah Mabao
  JEZI namba 11 ya Yanga anavaa Said Bahanuzi ‘Spider Man’ na jezi namba 11 ya Simba anavaa Abdallah Juma ‘Dullah Mabao’. Hadi sasa, katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame yanayoendelea mjini Dar es Salaam, Bahanuzi amekwishafunga mabao manne kwenye mechi tatu, wakati Abdallah amefunga mawili katika mechi mbili. Leo, Dullah Mabao anacheza mechi ya tatu na ya mwisho ya kundi lao, A dhidi ya AS Vita ta Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)- bila shaka anaweza kutikisa nyavu tena na kujiimarisha katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu cha mashindano haya. BIN ZUBEIRY inakuambia endelea kuwafuatilia vijana hawa katika mashindano hayo. Wote wanavaa jezi namba 11. Leo uwanjani tupia jicho lako katika jezi 11. Siku Yanga ikicheza tupia jicho kwa jezi 11.
  11 ya Yanga anavaa Spider Man
  Abdallah Juma
  Said Bahanuzi

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHUNGA SANA JEZI 11 SIMBA NA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top