Tetesi za J'tatu magazeti ya Ulaya


HATIMAYE MAN UNITED YAMNASA LUCAS MOURA KWA PAUNI MILIONI 26


KLABU ya Manchester United imekubali kutoa dau la pauni Milioni 26 kuinunua saini ya kinda Mbrazil, Lucas Moura, mwenye umri wa miaka 19, kutoka Sao Paulo.
Lucas Moura
Moura yuko na Brazil kwenye Olimpiki ya London 2012.
MAN United pia iko tayari kumsajili nyota wa Fulham, Moussa Dembele, mwenye umri wa miaka 25.
KLABU ya Arsenal inataka mshambuliaji wake anayetaka kuhama, Robin van Persie adai pauni Milioni 10.1 kwa mwaka, iwe Manchester United, City au Juventus ambazo zote zinamtaka Mholanzi huyo.
KLABU ya Manchester City imetega mitego yake kwa Daniele De Rossi, mwenye umri wa miaka 28, kwa mara nyingine tena baada ya kushindwa kumpata Mtaliano huyo msimu uliopita.
KLABU ya Tottenham anamtaka mshambuliaji wa AS Roma, Marco Borriello, mwenye umri wa miaka 30, baada ya kuambiwa hawana nafasi ya kumsajili nyota wa Atletico Madrid, Adrian Lopez.
Luka Modric
Modric anataka kuhamia Real Madrid
MCHEZAJI mwenye mkataba na Blackburn Rovers, Junior Hoilett hatajiunga na Queens Park Rangers, vinginevyo klabu hiyo ya London ilipe dau la pauni Milioni 6 au pendekezo la kubadilishana na Jamie Mackie.
KLABU mpya katika Ligi Kuu ya England, Southampton inataka kumsajili beki wa Blackburn, Scott Dann, mwenye umri wa miaka 25.
KLABU ya Fulham imempata kwa mkopo wa muda mrefu mshambuliaji wa Chelsea mwenye thamani ya pauni Milioni 18, Romelu Lukaku, mwenye umri wa miaka 19.
KLABU ya Crystal Palace inaweza kuendelea kuboresha kikosi chake kwa kumsajili mshambuliaji wa KIfaransa, Alexis Allart,mwenye umri wa miaka 25, ambaye atawagharimu pauni 300,000

AVB AKERWA NA MODRIC

KOCHA wa Tottenham, Andre Villas-Boas amekerwa na kitendo cha kiungo anayetaka kuhama klabu hiyo, Luka Modric raia wa Croatia kutoonekana mazoezini .
MWENYEKITI mwenye hasira kali nwa Spurs, Daniel Levy anaweza kuzuia uhamisho wowote wa Luca Modric baada ya mchezaji hujyo kutoonekana mazoezini mwishoni mwa wiki na atamtoza faini mchezaji huyo kwa mara ya tatu ndani ya siku nne ikiwa atashindwa kuhudhuria mazoezi na leo.

BALOTELLI ANAKUFURU JAMANI..

MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Mario Balotelli, mwenye umri wa miaka 21, amevunja rekodi ya matumizi kwa jinsi anavyotumia katika holiday yake huko Ibiza na kulipa 'bill' kubwa kubwa.