Tetesi za Ijumaa magazeti Ulaya


WENGER SASA AAMUA KUBOMOA BENKI, MAN UNITED YASAJILI KIUNGO MKENYA


Arsenal inamtaka mchezaji mwenye thamani ya pauni Milioni 20, Santi Cazorla, mwenye umri wa miaka 27, kiungo mchezeshaji kwa ajili ya msimu ujao - na bado wanamfukuzia kiungo wa Rennes, Yann M'Vila, mwenye umri wa miaka 22 na kinda la miaka 17, mshambuliaji wa Caen, M'Baye Niang.
AC Milan na Real Madrid zinajipanga kwa vita ya ana kwa ana ya kuwania saini ya beki wa Manchester City, Micah Richards mwenye umri wa miaka 24.
Liverpool imepiga hatua nzuri katika kuwania saini ya winga wa Bologna na Uruguay, Gaston Ramirez mwenye umri wa miaka 21, baada ya wakala wake kuwasili England kwa mazungumzo.
Gaston Ramirez
Gaston Ramirez aliifungia Uruguay katika mechi ya ufunguzi ya Olimpiki
Chelsea inaweza kutoa dau kununua mchezaji kwa mara ya nne, baada ya Marseille ya Ufaransa kusema beki wa kulia, Cesar Azpilicueta, mwenye umri wa miaka 22anaweza kuhama.
Liverpool inataka kuipiga chini ofa ya West Ham ya pauni Milioni 17 kwa ajili ya mshambuliaji wao mwenye umri wa miaka 23. Habari kamili: Daily Mail
Manchester United na Arsenal zina nia ya kumsajili kiungo mkabaji Mkenya, Victor Wanyama kutoka Celtic.
MWENYEKITI wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge amezitupilia mbali taarifa zinazowahusisha na kiungo wa Manchester City, Nigel de Jong mwenye umri wa miaka 27.
Lucas Moura
Lucas kwa sasa yuko England nas kikosi cha Brazil kinachoshiriki Olimpiki
NYOTA wa Brazil, Ganso, mwenye umri wa miaka 22, yuko tayari kuachana na ofa za Arsenal na AC Milan ili abaki Santos, licha ya kukataa kusaini mkataba mpya.
KLABU ya West Brom inakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Everton katika kuwania saini ya beki wa Villarreal, Cristian Zapata.

KOMPANY AKATAA OFA BARCA, REAL

Vincent Kompany amepuuza ofa za Real Madrid na Barcelona kabla ya kusaini kwa dau la rekodi, pauni Milioni 60 kujiunga na Man City
Atletico Madrid itampa ofa kiungo kinda, Oliver Torres kama motisha ya kumfanya apuuze ofa ya Chelsea.
BEKI wa kushoto wa England, Ashley Cole bado hajapatiwa  mkataba mpya, licha ya kwamba amebakiza mwaka mmoja.