• HABARI MPYA

  Tuesday, July 31, 2012

  KIPA WA SERENGETI BOYS YA SOMALIA AUAWA     
  KIPA wa kwanza wa timu ya taifa ya Somalia chini ya umri wa miaka 17, Abdulkader Dheere Hussein ameuawa mjini Mogadishu na watu wasiojulikana, Shirikisho la Soka Somalia (SFF) limesema.
  Kipa huyo kijana, aliuawa katika Wilaya ya Waberi mjini Mogadishu, baada ya kutokea mazoezini. “Bado hatujui nani alikuwa nyuma ya mauaji haya, lakini shirikisho la soka Somalia inafanyia uchunguzi suala hilo, ili kujua nani haswa alihusika na mauaji huyo.
  Katibu Mkuu wa SFF, Jenerali Abdi Qani Said Arab amesema katika taarifa yake ya Julai 26.
  Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa Hayatou amesikitishwa na mauaji hayo na kutoa salamu za pole kwa familia ya marehemu na wapenzi wa soka Somalia. Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amiin.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIPA WA SERENGETI BOYS YA SOMALIA AUAWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top