• HABARI MPYA

  Sunday, July 29, 2012

  RAIS MAZEMBE AFICHUA KINACHOMKWAMISHA ULIMWENGU


  Rais wa Mazembe, Moise Katumbi

  Na Prince Akbar
  MAKAMU wa Rais wa Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mohamed Kamwanya amesema kwamba Thomas Emmanuel Ulimwengu anachelewa kuingizwa kwenye kikosi cha kwanza kwa sababu kiwango chake bado.
  Thomas Ulimwengu
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY kwa simu kutoka Lubumbashi jana, Kamwanya alisema kwamba, Ulimwengu kila anapopewa ruhusa ya kurejea Tanzania kujiunga na timu za taifa, kwanza huchelewa kurudi Lubumbashi na pia hurudi akiwa hayuko fiti.
  “Hicho ndio kinamchelewesha, lakini kama siyo hivyo angekuwa anacheza tu kama mwenzake. Na nyinyi watu wa vyombo vya habari mtusaidie, kwa sababu wachezaji wakija huko wanafanya anasa, wanarudi huku hawako fiti, sasa inakuwa mbaya,”alisema Kamwanya.
  Akiwa anaingia msimu wa pili tangu asajiliwe na Mazembe, lakini Ulimwengu bado yupo kwenye kikosi cha wachezaji wa akiba wa timu hiyo na hachezi Ligi Kuu wala Ligi ya Mabingwa, kama mwenzake Mbwana Ally Samatta ambaye anang’ara.
  Akimzungumzia Samatta juu ya habari kwamba kuna klabu zinamataka Ulaya, Kamwanya alisema kwamba hadi sasa Mazembe haijapokea ofa yoyote kutoka kwa wakala au klabu na hawawezi kujadili mambo yanayozungumzwa au kuandikwa kama tetesi.
  “Tutakuwa tayari kusema, iwapo tutapata ofa ya maandishi, lakini kwa sasa tunasema Samatta tupo naye tu ni mchezaji wetu tegemeo,”alisema Kamwanya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS MAZEMBE AFICHUA KINACHOMKWAMISHA ULIMWENGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top