• HABARI MPYA

  Saturday, July 21, 2012

  SIMBA NA AZAM, YANGA NA MAFUNZO ROBO FAINALI KAGAME


  Sunzu kushoto na Kapombe kulia wakimpongeza Boban  Mudde akimpongeza Boban
  Na Prince Akbar
  SIMBA imetoka sare ya 1-1 na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),  katika mchezo wa mwisho wa Kundi A, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Katika mchezo huo, Felix Sunzu alikosa penalti dakika ya kwanza ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida, kufuatia beki mmoja wa Vita kuunawa mpira kwenye eneo la hatari, lakini shuti lake lilipanguliwa na kipa Mcameroon, Lukong Nelson kabla ya mabeki wake ‘kuosha’.
  Hadi mapumziko, Vita walikuwa mbele kwa bao 1-0, lilifungwa kwa penalti na Etikiama Taddy, dakika ya 35, baada ya Juma Said Nyosso kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
  Simba ilisawazisha bao hilo kupitia kwa Haruna Moshi ‘Boban’ aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Patrick Kanu Mbivayanya dakika ya 66.
  Katika mchezo huo, Simba ilipata pigo dakika ya 27, baada ya mshambuliaji wake Abdallah Juma ‘Dullah Mabao’ kuumia kifundo cha mguu na kutoka nje, nafasi yake ikichukuliwa na Kiggi Makassy.
  Kwa matokeo hayo, Simba imemaliza kama mshindi wa tatu katika Kundi A na itamemnyana na Azam katika Robo Fainali Jumanne, wakati mabingwa watetezi Yanga watamenyana na Mafunzo Jumatatu.
  Robo Fainali nyingine zitakuwa kati ya URA na APR na Atletico dhidi ya Vita.
  Simba SC; Juma Kaseja, Haruna Shamte, Shomary Kapombe, Lino Masombo, Juma Nyosso, Mussa Mudde/Salim Kinje, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Abdallah Juma na Kanu Mbivayanga/Haruna Moshi.
  AS Vita; Lukong Nelson, Ilo ngo Ilifo, Issama Mpeko, Ebunga Simbi, Mutombo Kazadi, Lema Mabidi, Etekiama Taddy, Mapuya Lema, Magola Mapanda, Basilua Makola, Mfongang Alfred.
  KIggi anatia krosi

  Kipa wa Vita akiruka bila mafanikio kuokoa shuti la Boban lililotinga nyavuni

  RATIBA ROBO FAINALI
  Julai 23, 2012
  Mafunzo vs Yanga
  URA vs APR
  Julai 24, 2012
  Atletico vs AS Vita
  Azam vs Simba SC
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA NA AZAM, YANGA NA MAFUNZO ROBO FAINALI KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top