• HABARI MPYA

  Saturday, July 21, 2012

  AZAM YAIBEBA MAFUNZO ROBO FAINALI KAGAME

  Kikosi cha Azam leo


  Kikosi cha Tusker leo


  Na Prince Akbar
  AZAM na Mafunzo ya Zanzibar zimefuzu kuingia Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, kufuatia Wana Chamazi kutoka sare ya bila kufungana na Tusker ya Kenya mchana wa leo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Timu zote za Kundi B zimemaliza zikiwa na pointi mbili kila moja, lakini Tusker haina bao baada ya kutoa sare ya bila kufungana mechi zote na Mafunzo na Azam wanabebwa na sare ya kufungana bao 1-1 katika mechi ya kwanza kabisa ya kundi hilo, Uwanja wa Chamazi.
  Tusker walilazimika kucheza pungufu tangu dakika ya 51, baada ya kipa wao Boniphace Olouch kutolewa nje kwa kadi nyekundu na refa Issa Kagabo wa Rwanda kwa kumchezea rafu John Bocco wakati anakwenda kufunga.
  Andrew Mutunga alitoka na akaingia kipa wa akiba Samuel Odhiambo na katika kuogeza kasi ya mashambulizi, Azam walimpumzisha Kipre Tchecthe akaingia Mrisho Ngassa.
  Katika mchezo huo, kikosi cha Azam kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Ibrahim Shikanda, Jospeh Owino, Kipre Ballou, Kipre Tchetche, Ibrahim Mwaipopo, John Bocco, Ramadhan Chombo na Hamisi Mcha ‘Vialli’.
  Benchi; Mwadini Ally, Samir Hajji Nuhu, Said Mourad, George Odhiambo ‘Blackberry’, Mrisho Ngassa, Jabir Azizi na Gaudence Mwaikimba.
  Kocha; Stewart Hall (Uingereza)  
  Tusker; Boniface Oluouch, Joseph Shikokoti, Jockins Atudo, Humphrey Okoti, David Ochieng, Joseph Mbugi, David Nyanzi Makumbi, Jerry Santo, Andrew Murunga, Peter Opiyo na Joshua Oyoo.
  Benchi; Samuel Odhiambo, Luke Ochieng, Maurice Odipo, Dennis Mukaisi, Fredrcik Onyango, Patrick Kagogo, Obadia Ndege, Joseph Mbugi na Allan Kateregga.
  Kocha; Samuel Omollo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM YAIBEBA MAFUNZO ROBO FAINALI KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top