• HABARI MPYA

  Tuesday, July 24, 2012

  COASTAL UNION YASAJILI MTOTO WA MAXIMO

  KIUNGO wa kimataifa wa Zanzibar, Suleiman Kassim ‘Selembe’ akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union ya Tanga, Steven Mnguto hivi karibuni. Kwa mujibu wa facebook page ya Coastal, mabingwa wa 1988 wa Ligi Kuu, wamemsajili kiungo huyo aliyechezea kwa mkopo African Lyon ya Dar es Salaam msimu uliopita akitokea Azam na wakaamua kumpeleka Mafunzo acheze Kombe la Kagame kwa ajili ya kuongeza idadi ya mechi za kimataifa kwake.
  Coastal wametamba, kutokana na kasi ya Selembe, akili ya kisoka, wepesi na mashuti yake, ataifanya Coastal iwe tishio msimu ujao.
  Selembe ni miongoni mwa ‘makinda’ ya mwishoni kutengenezwa na aliyekuwa kocha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbrazil Marcio Maximo.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL UNION YASAJILI MTOTO WA MAXIMO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top