• HABARI MPYA

  Tuesday, July 24, 2012

  NGASSA AWANUNIA WOTE AZAM KUSHINIKIZA KUREJEA YANGA, LAKINI AAMBIWA ATAJIJU CHAMAZI TU


  USO WA MBUZI; Ngassa akiwa kwenye benchi la wachezaji wa akiba Azam kama hahusiki vile 

  KOCHA wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall amesema hamtumii Mrisho Khalfan Ngassa kwa sasa, kwa sababu haonyeshi dalili za kutaka kucheza.
  “Hana jitihada zozote, hajitumi, hana hamu ya kucheza, siwezi kumchezesha,”alisema Stewart mapema tu, kabla ya mechi ya Robo Fainali dhidi ya Simba SC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Pamoja na kucheza bila Ngassa, Azam imeshinda 3-1 na kuingia Nusu Fainali, ambako itamenyana na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Kuna tetesi kwamba, Ngassa yupo kwenye mgomo baridi kushinikiza uhamisho wa kurejea Yanga, lakini habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata kutoka ndani ya Azam, zinasema kwamba, klabu hiyo itaendelea kuishi naye hivyo hivyo ‘kimakunyanzi’ hadi amalize mkataba wake msimu ujao. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGASSA AWANUNIA WOTE AZAM KUSHINIKIZA KUREJEA YANGA, LAKINI AAMBIWA ATAJIJU CHAMAZI TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top