• HABARI MPYA

  Sunday, July 22, 2012

  SAMATTA KUENDELEA KUTIKISA NYAVU AFRIKA LEO?

  Mshambuliaji chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ‘Sama Goal’ (pichani), leo anatarajiwa kuiongoza klabu yake, Tout Puissant Mazembe mjini Lubumbashi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Berekum Chelsea ya Ghana, kuanzia saa10:30 jioni. Mechi nyingine ya Kundi lao, itakuwa ni kati ya wapinzani wa jadi katika soka ya Misri, Zamalek na Al Ahly, kuanzia saa 5:00 usiku. Mbwana, au Poppa kama wamuitavyo nyumbani Mbagala, aliiambia BIN ZUBEIRY juzi kwa simu kutoka Lubumbashi, kwamba yuko fiti na anaamini ataanza- akaomba Watanzania wamuombee dua aendelee kung’ara Afrika. Katika mechi ya kwanza ugenini dhidi ya Ahly, Samatta aliifungia bao Mazembe.

  Hapa Samatta akiichezea Taifa Stars dhidi ya Ivory Coast mjini Abidjan miezi miwili iliyopita. Hapa anapambana na Kolo Toure wa Manchester City katika mechi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2012. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA KUENDELEA KUTIKISA NYAVU AFRIKA LEO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top