• HABARI MPYA

  Thursday, July 26, 2012

  AZAM WATANGULIA FAINALI, NGASSA AWAZAWADIA BAO YANGA


  Ngassa akishangilia bao lake la mashabiki wa Yanga

  NUSU Fainali ya kwanza ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, michuano inayodhaminiwa na Super Sport na Azam, imemalizika kwa Azam FC kuitoa AS Vita kwa kuifunga mabao 2-1, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Hadi mapumziko, AS Vita walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililofungwa na Mfongang Alfred dakika ya 34, baada ya kuunasa mpira uliopigwa na Ibrahim Shikanda na kuichambua ngome ya Azam kabla ya kufumua shuti kali lililomshinda kipa Deo Munishi ‘Dida’.
  Vita walipata pigo dakika ya 41, baada ya mchezaji wao, Issama Mpeko kutolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja.
  Azam ilisawazisha bao hilo, kupitia kwa John Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 68 aliyeunganisha kwa kichwa krosi ya Kipre Tchetche kutoka wingi ya kulia.
  Mrisho Khalfan Ngassa aliyeingia kutokea benchi kipindi cha pili aliifungia Azam bao la ushindi dakika ya 89, akimalizia pasi ya Salum Abubakar ‘Sure Boy’. Baada ya kufunga bao hilo, Mrisho alikwenda moja kwa moja kwan mashabiki wa Yanga na kushangilia nao, badala ya mashabiki wa Azam.
  Nusu Fainali ya pili kati ya mabingwa watetezi, Yanga na APR ya Rwanda ndio inaendelea hivi sasa na mshindi atamenyana na Azam. Azam inakuwa timu ya pili nje ya Simba na Yanga kuingia Fainali ya michuano hii, baada ya mwaka 2006 Moro United kufanya hivyo.
  Kikosi kilichoipeleka Azam Nusu Fainali

  John Bocco akishangilia bao lake

  Mpira nyavuni- Bocco

  Angalia vikosi;
  Azam FC; Deo Munishi ‘Dida’, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey Morris, Jabir Aziz, Kipre Tcheche, Salum Abubakar, John Bocco ‘Adebayor’, Ibrahim Mwaipopo na Ramadhan Chombo ‘Redondo’.
  Benchi; Mwadini Ally, Samir Haji Nuhu, Joseph Owino, George Odhiambo, Mrisho Ngassa, Khamis Mcha ‘Vialli’ na Gaudence Mwaikimba.
  Kocha; Stewart Hall (Uingereza)   
  AS Vita; Lukong Nelson, Ilongo Ilifo, Issama Mpeko, Ebunga Simbi, Mapuya Lema, Mfongang Alfred, Niemba Nkanu, Magola Mapanda, Mutombo Kazadi, Lema Mubidi na Etekiama Taddy.
  Benchi; Matadi Mankutima, Ngudikama Emmanuel, Ngoyi Emomo, Romaric Rugombe, Basilua Makola, Tshimanga Mutamba na Pambanio Makiadi.  
  Kocha; Raoul Shungu (DRC)
  Kikosi cha Yanga kilichoanza

  MECHI YA PILI;
  Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Godfrey Taita, Haruna Niyonzoma, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na David Luhende.
  Benchi; Yaw Berko, Rashid Gumbo, Stefano Mwasyika, Shamte Ally, Ladislaus Mbogo, Juma Seif na Idrissa Rashid.   
  APR; Jean Ndoli Claude, Olivier Karekezi, Suleiman Ndikumana, Mugiraneza Jean, Johnson Bogoole, Lonel St Preus, Ngabo Albert, Iranzi Jean Claude, Mbuyu Twite, Dan Wagaluka na Tuyizere Donatien.
  Benchi; Ndayishimye Jean Luc, Nova Bayama, Ngomirakiza Herman, Ernest Kwizera, Habib Kavuma, Mubumbyi Barnabe na Sekamana Maxime.
  Kocha; Ernest Brandy (Uholanzi)    

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM WATANGULIA FAINALI, NGASSA AWAZAWADIA BAO YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top