• HABARI MPYA

  Monday, July 30, 2012

  MESSI WA SIMBA AAMINI NIGERIA WATAKUFA KWAO


  Messi wa Msimbazi katika mechi ya jana

  Na Prince Akbar
  KIUNGO Ramadhani Singano ‘Messi’, chipukizi wa timu ya taifa hya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes anayechezea klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam, amesema kwamba uwezo wa kuwafunga Nigeria 2-0 wiki ijayo kwao na kusonga mbele kwenye Fainali za Afrika upo, iwapo watafanyia vema makosa yao.
  Mabao mawili ya Achaji Gero jana yaliiwezesha Flying Eagles kuifunga Ngorongoro Heroes mabao 2-1 katika mechi ya kwanza ya Raundi ya Pili, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika.
  Mshambuliaji huyo mrefu wa Enugu Rangers, alifunga mabao yake katika dakika ya pili na 44 jana, kabla ya Ngorongoro kupata bao la kufutia machozi, lililofungwa na Atupele Green dakika ya 50, akimalizia krosi ya Messi wa Msimbazi.
  “Kama umeona kipindi cha pili tulitulia na tulitawala mchezo, tulitengeneza nafasi nyingi, lakini tukatumia moja tu. Na hatukuwapa nafasi kabisa kumiliki mpira. Sasa kama mechi ya marudiano tutacheza hivyo, tunaweza kuwafunga 2-0 na tukasonga mbele.
  Cha msingi ni kutokata tamaa, turudi kambini mapema ili tuanze maandalizi, naamini nafasi bado tunayo,”alisema Messi.
  Baada ya mechi ya marudiano na Nigeria, Messi anatarajiwa kwenda Austria kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa, nchi ambayo tayari mshambuliaji wa Simba, Mganda Emmanuel Okwi yuko akiendelea na majaribio pia.
  Wakati Okwi atanunuliwa kwa Euro 600,000 akifuzu, Messi atanunuliwa kwa dola za Kimarekani 300,000 akifuzu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MESSI WA SIMBA AAMINI NIGERIA WATAKUFA KWAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top