• HABARI MPYA

    Monday, July 23, 2012

    NI YANGA NA APR TENA NUSU FAINALI

    MAHADHI MPYA; Kipa wa Mafunzo, Halid Mahadhi Haji akidaka mpira mbele ya mshambuliaji wa Yanga, Said Bahanuzi

    Yanga


    Mafunzo
    YANGA imefuzu kuingia Nusu Fainali ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, baada ya kuifunga Mafunzo ya Zanzibar kwa penalti 5-3, kufuatia sare bya 1-1 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wawakilishi wa Zanzibar Mafunzo walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Ali Othman Mmanga, dakika ya 34, akiunganisha kona ya Juma Othman Mmanga na Yangab wakasawazisha dakika ya 46, mfungaji Said Bahanuzi ‘Spider Man’.
    Yanga sasa itamenyana na APR ya Rwanda, keshokutwa ambayo katika Robo Fainali ya kwanza, imeitoa URA ya Uganda kwa kuifunga 2-1, mabao yake yakifungwa na Jean Claude Iranzi dakika ya tisa na Suleiman Ndikumana dakika ya 34, wakati la Watoza Ushuru wa Kampala, lilifungwa na Robert Ssentongo dakika ya 57.
    Yanga SC; Yaw Berko, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Stefano Mwasyika, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na Rashid Gumbo.
    Benchi; Ally Mustafa ‘Barthez’, Shamte Ally, Ladislaus Mbogo, Godfrey Taita, Juma Seif ‘Kijiko’, Jerry Tegete na Idrisa Rashid.
    Mafunzo; Khalid Mahadhi Hajji, Ismail Khamis Amour, Said Mussa Shaaban, Salum Said Shebe, Ali Othman Mmanga, Juma Othman Mmanga, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Jaku Juma Jaku, Mohamed Abdulrahim, Wahid Ibrahim na Ally Juma Hassan.
    Benchi; Salum Mohamed Pangani, Hajji Abdi Hassan, Kheir Salum Kheir, Sadik Habib Rajab  na Thabit Mohamed Abdallah.

    MECHI YA KWANZA....
    Wachezaji wa APR wakimpongeza Ndikumana, aliyeinua vidole juu kushoto kwa kufunga bao la pili

    Dan Wagaluka wa URA kushoto akitafuta mbinu za kumtoka beki wa APR kulia

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NI YANGA NA APR TENA NUSU FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top