• HABARI MPYA

    Sunday, July 29, 2012

    NGORONGORO NA NIGERIA LEO TAIFA BONGE LA GAME


    Kikosi cha Ngorongoro cha mwaka juzi

    Na Prince Akbar
    TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes leo inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kumenyana na vijana wenzao wa Nigeria, Flying Eagles katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya pili kuwania kucheza Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri huo, zitakazofanyika mwakani nchini Algeria.
    Kocha Mkuu wa Ngorongoro Heroes, Menmark Jakob Michelsen na Nahodha wa timu hiyo, kiungo Omega Seme wamesema timu yao iko tayari kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Kenya.
    Michelsen amesema timu yake imepata mechi mbili za kujipima nguvu dhidi ya Rwanda, lakini pia aliishuhudia Flying Eagles ikicheza mechi ya kirafiki na Rwanda (Young Amavubi) uliofanyika Julai 24 mwaka huu jijini Kigali.
     “Timu iko vizuri na wachezaji kama Frank Domayo, Simon Msuva na Ramadhan Singano ambao pia wanachezea timu A (Taifa Stars), hivyo uzoefu wao ni muhimu kwa mechi ya kesho.
    “Nigeria ni mabingwa watetezi wa michuano hii kwa hiyo tunatarajia upinzani mkubwa, lakini tumejiandaa kwa hilo. Nigeria ni nchi yenye mfumo mzuri wa timu za vijana, na sisi tunaelekea huko huko” amesema Michelsen.
    Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Flying Eagles, John Obuh amesema haijui vizuri Ngorongoro Heroes lakini anaiheshimu kutokana na ukweli kuwa inacheza raundi ya pili baada ya kuitoa Sudan katika raundi ya kwanza.
    “Sina mchezaji yeyote anayecheza mpira wa kulipwa nje ya Nigeria, lakini tumekuja kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kucheza raundi ya mwisho na hatimaye tucheze fainali mwakani,” amesema Obuh aliyefuatana na nahodha wake Samuel Okan ambaye ni mlinda mlango.
    Katika mechi hiyo, itakayochezeshwa na refa Moses Osano, akisaidiwa na Peter Keireni na Elias Wamalwa, Thomas Onyango mezani, viingilio vitakuwa Sh. 3,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani wakati VIP B na C itakuwa sh. 5,000. Kiingilio kwa VIP A ni sh. 10,000.
    Osano atasaidiwa na Peter Keireini na 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGORONGORO NA NIGERIA LEO TAIFA BONGE LA GAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top