• HABARI MPYA

  Saturday, July 21, 2012

  MATUTA YAWAKOSESHA MWALI MAKINDA WA COASTAL UNION BURUNDI


  Nassor Binslum

  Na Prince Akbar
  TIMU ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Coastal Union ya Tanga, leo imeshindwa kutwaa Kombe la Rollingston, baada ya kufungwa kwa penalti 4-2 katika fainali nchini Burundi leo, kufuatia sare ya ndani ya dakika 120.
  Kwa mujibu wa Nassor Binslum, mfadhili wa timu hiyo, Coastal Union ilimiliki mpira kwa kiasi kikubwa na kukosa mabao mengi ya wazi, wakati wapinzani wao walitumia mbinu ya ‘kupaki basi’ hatimaye wakabahatisha sare ndani ya dakika 120.
  Ikumbukwe, Coastal ilifanikiwa kuingia fainali ya michuano ya Rollingston, baada ya kuwafunga mabingwa watetezi, Ruvu Shooting mabao 2-1 nchini Burundi.
  Mabao yote ya Coastal siku hiyo yalitiwa kimiani na Mohamed Miraj, wakati bao la Ruvu waliotwaa ubingwa wa michuano hiyo mwaka jana mjini Arusha, lilitiwa kimiani na Said Hussein.
  Coastal inatarajiwa kuondoka kesho Burundi kurejea Dar es Salaam na Medali yao ya Fedha kutoka kwenye michuano hiyo, ambayo awali ilikuwa inafanyika nchini Burundi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MATUTA YAWAKOSESHA MWALI MAKINDA WA COASTAL UNION BURUNDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top