• HABARI MPYA

    Monday, July 30, 2012

    YANGA WAACHIA BONGE LA STRIKER WALILOSAJILI KWA PESA NDEFU, COASTAL WAJIBEBEA KIULAINIIIIIII


    Green kulia katika mechi ya jana

    Na Prince Akbar
    MWAKA 2010, Atupele Green aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa akademi au timu ya vijana kusajiliwa kwa bei mbaya zaidi katika soka ya Tanzania, baada ya kusajiliwa na Yanga kwa Sh. Milioni 27, enzi hizo Katibu Mkuu, Lawrence Mwalusako na Kocha Mkuu Kosatadin Papic, Meneja Emmanuel Mpangala.
    Lakini tangu asajiliwe, Green hajawahi kuchezea kikosi cha wakubwa cha Yanga na sasa inaelezwa mchezaji huyo amesajiliwa Coastal Union ya Tanga, kama mchezaji huru, kwa kuwa amekwishamaliza makataba wake Jangwani.
    Kwa sasa Green, ndiye mshambuliaji tegemeo wa timu ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes ambayo jana ilifungwa mabao 2-1 nyumbani na Nigeria katika mechi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana.
    Achaji Gero wa Enugu Rangers, wapinzani wa zamani wa Yanga, ndiye aliyefunga mabao yote mawili ya Flying Eagles, wakati Green alifunga bao la kufutia machozi la Ngorongoro.
    Wakati Yanga ikimuacha Green akienda Coastal, yenyewe imevunja benki yake na kusajili wachezaji wawili wa Ngorongoro, kiungo Frank Damayo na mshambuliaji wa pili, Simon Msuva.  
    Katika Ngorongoro ya sasa, Green na Msuva wanacheza kama washambuliaji pacha, wakicheza kwa uelewano mkubwa na kiungo mshambujliaji, Ramadhani Singano ‘Messi’.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA WAACHIA BONGE LA STRIKER WALILOSAJILI KWA PESA NDEFU, COASTAL WAJIBEBEA KIULAINIIIIIII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top