• HABARI MPYA

  Saturday, July 21, 2012

  HUYU NDIYE KOCHA WA AS VITA ALIYEONEKANA WA KAZI KAZI YANGA

  Kocha wa AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Raoul Jean Pierre Shungu aliyewahi kuinoa Yanga (1998-2001).  Shungu alifukuzwa Yanga, enzi hizo Mwenyekiti Tarimba Abbas, akaenda Mtibwa Sugar, ambako baada ya msimu mmoja akaenda Rwanda, Shelisheli na sasa yuko nyumbani kwao, DRC. Vita leo imetoka 1-1 na Simba SC leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Hadi sasa, Vita ndiyo timu inayosifika kwa kuongoza kwa kandanda ya kuvutia zaidi katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki, Kombe la Kagame inayoendelea nchini. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HUYU NDIYE KOCHA WA AS VITA ALIYEONEKANA WA KAZI KAZI YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top